Misri yakosoa hatua ya baadhi ya nchi katika kuunga mkono ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27678-misri_yakosoa_hatua_ya_baadhi_ya_nchi_katika_kuunga_mkono_ugaidi
Waziri Mkuu wa Misri amezituhumu baadhi ya nchi waungaji mkono wakubwa wa makundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2017 09:41 UTC
  • Misri yakosoa hatua ya baadhi ya nchi katika kuunga mkono ugaidi

Waziri Mkuu wa Misri amezituhumu baadhi ya nchi waungaji mkono wakubwa wa makundi ya kigaidi.

Sherif Ismail ameyasema hayo akihutubia bunge la Misri ambapo bila kutaja majina ya nchi hizo za kigeni katika kuunga mkono ugaidi, amesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi nchini humo yaliratibiwa na baadhi ya nchi hizo.

Ali Abdel Aal Spika wa Bunge la Misri

Wakati huo huo, Ali Abdel Aal Spika wa Bunge la Misri amesema kuwa, baada ya kujiri miripuko katika makanisa mawili nchini humo, serikali imebaini kwamba magaidi waliotekeleza hujuma hizo, walipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa baadhi ya nchi za nje. Amesema kuwa, ushahidi unaonyesha kwamba uungaji mkono huo uliwawezesha magaidi kutumia zana za kisasa katika kufanikisha mashambulizi hayo. Jumanne ya jana bunge la Misri lilipitisha muswada unaohusiana na hali ya hatari ya miezi mitatu ndani ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika. Hali hiyo ya hatari inavijumuisha pia vyombo vya habari na magazeti.

Baada ya mpripuko kutokea nchini Misri

Katika hujuma za kigaidi dhidi ya makanisa mawili ya mji wa Tanta na Alexandria, kaskazini mwa nchi, ambazo zilipelekea karibu watu 50 kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa, kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) lilitangaza kuhusika na jinai hiyo.