May 21, 2017 03:33 UTC
  • AU yataka msaada wa kimataifa kukabiliana na waasi wa Kikristo wa LRA

Umoja wa Afrika umetoa wito wa msaada wa kijeshi wa kimataifa kukabiliana na waasi wa Kikrsito wa LRA kutoka Uganda walio katika misitu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiongozwa na Joseph Kony.

Hatua hiyo imefuata uamuzi wa Uganda na Marekani kuondoa wanajeshi waliokuwa wakiwasaka waasi hao huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mwezi Aprili Jeshi la Ulinzi la Uganda UPDF lilianza kuondoa askari wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao wamekuweko nchini humo tangu mwaka 2012.

Kwa mujibu wa taarifa ya UPDF, uamuzi huo wa Uganda kuanza kuondoa vikosi vyake Jamhuri ya Afrika ya Kati umetokona na ukweli kwamba, jeshi la Uganda limefanikiwa pakubwa kuzima harakati za kundi la waasi la LRA kiasi kwamba, haliwezi kuanzisha vita vyovyote dhidi ya Uganda.

Mwezi Machi pia Marekani ilitangaza kuaondoa askari 100 ambao walikuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa madai ya kuwasaka waasi hao wa LRA. Kiongozi wa LRA Joseph Kony anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu.

Waasi wa LRA

Hadi sasa vikosi vya Marekani, Uganda, Jamhuri ya Kidemorsaia ya Kongo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati vimeshindwa kumkamata Kony. Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linasema LRA bado ni tishio na hivyo kunahitajika msaada ya haraka wa kijeshi ili kukabiliana na kundi hilo.

Kundi la waasi wa Kikristo la LRA liliasisiwa kaskazini mwa Uganda zaidi ya miongo miwili iliyopita kwa shabaha ya kuasisi utawala nchini humo uliosimama juu ya amri kumi za Biblia.

Waasi hao walipanua wigo wa harakati zao na kuvuka mpaka ambapo waliingia mashariki mwa Kongo na baadaye katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tags