Umoja wa Ulaya wazungumza na Tunisia kuhusu njia za kupambana na ugaidi
Maafisa wa kupambana na ugaidi wa Umoja wa Ulaya wameitisha kikao na viongozi wa Tunisia kujadiliana njia za kupambana na ugaidi.
Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa, Gilles de Kerchove, mratibu wa Umoja wa Ulaya katika vita dhidi ya ugaidi ameonana na viongozi wa Tunisia mjini Tunis na kujadiliana nao njia mbalimbali za kupambana na ugaidi ikiwa ni pamoja na kubadilisha taarifa za kijasusi za kulikabili janga hilo la dunia nzima.
Kershove amewaambia waandishi wa habari mjini Tunis kwamba, hivi sasa kuna mabadilishano mazuri ya taarifa baina ya viongozi wa Tunisia na ujumbe mbalimbali wa masuala ya usalama na mahakama wa Umoja wa Ulaya na jambo hilo linarahisisha kuchukuliwa hatua mwafaka za kukabiliana na ugaidi.
Viongozi wa nchi za Magharibi wanaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa wa kuenea vitendo vya kigaidi katika nchi zao. Hata hivyo ni nchi hizo hizo za Magharibi ndizo zilizoyaunda na kuyasaidia kwa kila namna magenge ya kigaidi katika nchi mbalimbali hasa Syria na Iraq.
Siku chache zilizopita, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ufaransa aliitwa mahakamani kujibu tuhuma za kushirikiana na magenge ya kigaidi nchini Syria hususan Daesh.
Kabla ya hapo, Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani, Hillary Clinton alikiri kwamba ni wao ndio waliounda genge la kigaidi la Daesh yaani ISIS.