Operesheni ya G5 dhidi ya ugaidi yaanza eneo la Sahel la Afrika
Askari wa nchi tano 'G 5' za eneo la Sahel la Afrika wameanza operesheni dhidi ya ugaidi katika eneo hilo.
Askari wa nchi hizo tano wameanza operesheni hiyo dhidi ya ugaidi karibu na mpaka wa pamoja kati ya Niger na Burkina Faso. Katika operesheni hiyo, askari kutoka Mali wamewekwa umbali wa kilometa chache kutoka mpaka wa Burkina Faso.
Kwa mara ya kwanza askari wa Mali, Burkina Faso na Niger watakuwa chini ya kamandi moja inayosimamiwa na kikosi hicho cha G5 cha eneo la Sahel la Afrika na kwa msingi huo, inakadiriwa kuwa wataweza kulinda vyema mipaka ya nchi zao. Kundi la askari hao linajumuisha askari kutoka mataifa ya Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad. Pendekezo la kuundwa kikosi hicho lilitolewa na Ufaransa kwa lengo la kupambana na ugaidi katika eneo la Afrika hususan katika eneo la Sahel.