Watanzania watakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki cha wimbi la lawama + Sauti
Mar 04, 2018 14:31 UTC
Watanzania wametakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho serikali ya nchi hiyo inatupiwa lawama na wanaharakati wa haki za kiraia, vyama vya upinzani, wananchi na vyombo vya habari kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa haki na demokrasia.
Wananchi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki aidha wametakiwa kudumisha utulivu na mshikamano ili kuendelea kuliweka taifa hilo katika amani na usalama.
Hayo yanajiri katika hali ambayo kumekuwa kukiripotiwa matukio tata ya mauaji na kutekwa raia huku vyama vya upinzani vikidai kwamba serikali inahusika katika matukio hayo.
Mwandishi wa Radio Tehran jijini Dar es Salaam ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo.
Tags