May 03, 2018 04:37 UTC
  • Watu 24 wauawa katika machafuko mapya Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Watu wasiopungua 24 wanaripotiwa kuuawa katika mapigano mapya yaliyozuka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Duru za hospitali kutoka Bangui zinaripoti kuwa, watu hao wameuawa katikka mapigano baina ya makundi yay wabeba silaha na vikosi mvya usalama yaliyozuka upya siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Mapigano hayo yamezuka baada ya mji wa Bangui kushuhudia hali ya amani na utulivu kwa miezi kadhaa sasa na kuleta matumaini ya kurejea tena amani na usalama katika mji huo.

Wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka

Mmoja wa viongozi wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, endapo watu wanaohusika na vitendo vya machafuko na mauaji hawatatiwa mbaroni, machafuko hayo mapya yatashadidisha mashambulio na mauaji.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ni moja ya nchi masikini zaidi duniani, ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé kufuatia hujuma ya waasi wa Seleka nchini humo.

Tangu wakati huo hadi sasa nchi hiyo imekuwa uwanja wa mapigano ya kila uchao kati ya makundi hasimu, hususan lile la Kikristo la Anti-Balaka na lile la Seleka. Hali hiyo imezidi kuisababishia matatizo mengi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tags