Jun 23, 2018 07:51 UTC
  • Mapigano yaendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mapigano ya ndani ya hivi karibuni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamepelekea kuuawa na kujeruhiwa watu wengi nchini humo.

Vyanzo vya kuaminika kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati viliripoti jana Ijumaa kwamba mapigano mapya yalizuka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumatano tarehe 20 Juni kati ya waasi wa zamani wa Seleka na wanamgambo wa Anti-Balaka karibu na mji wa Bria katikati mwa nchi hiyo. Hakuna idadi kamili iliyotolewa kuhusiana na wahanga wa mapigao hayo lakini vyanzo vya eneo la tukio vinasema mbali na waasi hao wa zamani na wanamgambo wa Anti-Balaka, kuna raia wengi waliouawa na kujeruhiwa katika mapigano hayo.

Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vladimir Monteiro, msemaji wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Afrika ya Kati Munisca amesema kikosi chake kilichukua uamuzi wa kutuma askari wa kupiga doria kusini mwa mji wa Bria hapo siku ya Ijumaa. Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tokea mwaka 2013.

Tags