Jul 24, 2018 03:25 UTC
  • Magaidi wa Boko Haram wahujumu msikiti na kuua watu wanane Nigeria

Magaidi wakufurishaji wa kundi la Boko Haram wameshambulia msikiti na kuua watu wanane mashariki mwa Nigeria.

Taarifa zinasema mlipuko ulitokea Jumatatu asubuhi  katika wilaya ya Mainari Konduga katika jimbo la Borno ambalo ni ngome ya magaidi wa Boko Haram.

Imearifiwa kuwa mshambuliaji aliingia msikitini wakati wa sala ya Alfajiri na kujjilipua katika umati wa waumini Waislamu waliokua katika sala ambapo watu wanane walipoteza maisha papo hapo na watano wakajeruhiwa.

Waislamu wa kaskazini mashariki mwa Nigeria ni waathirika wakuu wa ugaidi unaeondeshwa na magaidi wa Kiwahhabi ambao huwakufurisha Waislamu wote wasioafiki itikadi zao potovu na ni kwa msingi huo ndio magaidi hao huwa wanalenga misikiti.

Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Zaidi ya watu elfu 20 wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009 huku wengine zaidi ya milioni mbili wakilazimika kukimbia makazi yao kutokana na ugaidi wa Boko Haram ambao sasa umeenea katika nchi jirani kama vile Cameroon, Niger na Chad.

Tags