Sep 25, 2018 13:44 UTC
  • Al Sirraj aahidi kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi Libya

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amesema kuwa serikali yake itaandaa mazingira mazuri ya kufanyka uchaguzi licha ya mapigano yanayoendelea sasa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Fayez al Sirraj amesema kuwa mchakato wa kidemokrasia hautaishia kwenye Bunge la Libya lenye makao yake huko Tobruk. Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ameongeza kuwa, serikali yake itadhamini matakwa yote ya Tume Kuu ya Uchaguzi na kuandaa anga nzuri ya kufanyika uchaguzi katika mazingira ya amani na ya wazi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine husika za kimataifa. 

 Wakati huo huo Al Sirraj ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kivitendo ili kuhitimisha machungu na masaibu ya wananchi wa Libya.

Makundi ya Libya mwezi Mei mwaka huu yalikutana Paris na kufikia mapatano ya kuitisha chaguzi za rais na bunge nchini humo Disemba 10 mwaka huu.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa mji mkuu wa Libya, Tripoli wiki kadhaa za karibuni ulikumbwa na mapigano kati ya makundi ya waasi yenye mfungamano na serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo na kundi linaloitwa" Brigedi ya Saba." 

Makundi yenye silaha ya Libya 

 

Tags