Israel yaktaa kufichua nafasi yake katika mauaji ya kimbari ya Rwanda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4966-israel_yaktaa_kufichua_nafasi_yake_katika_mauaji_ya_kimbari_ya_rwanda
Mahakama ya Juu ya utawala wa kizayuni wa Israel imepitisha kuwa, nyaraka za mauzo ya silaha ya utawala huo haramu kwa serikali ya Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari katika nchi hiyo ya Kiafrika mwaka 1994, hazitawekwa wazi kwa wananchi na zitaendelea kufichwa na kubakia siri kuu ya utawala huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 13, 2016 02:55 UTC
  • Israel yaktaa kufichua nafasi yake katika mauaji ya kimbari ya Rwanda

Mahakama ya Juu ya utawala wa kizayuni wa Israel imepitisha kuwa, nyaraka za mauzo ya silaha ya utawala huo haramu kwa serikali ya Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari katika nchi hiyo ya Kiafrika mwaka 1994, hazitawekwa wazi kwa wananchi na zitaendelea kufichwa na kubakia siri kuu ya utawala huo.

Mahakama hiyo imesema kuwa, licha ya kuwa watu wa Israel wana haki ya kujua na kufahamishwa taarifa zote za utawala huo, lakini kufichua nyaraka hizo zinazobainisha namna Israel ilivyoiuzia silaha serikali ya wakati huo ya Rwanda wakati ya mauaji ya kimbari, ni hatari kwa usalama na sera za kigeni za utawala huo.

Ombi la kuutaka utawala haramu wa Israel ushurutishwe kuweka wazi nyaraka hizo liliwasilishwa katika Mahakama ya Juu na mwanasheria Eitay Mack na Profesa Yair Auron mwaka 2014. Wawili hao walitaka Wizara ya Vita ya Israel iagizwe kufichua mauzo ya silaha yake kwa serikali ya Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1995.

Katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mbali na watu wasiopungua laki nane kuuliwa, wanawake laki mbili pia walibakwa na kunajisiwa. Mauaji hayo yalianza baada ya kutunguliwa ndege iliyokuwa imewabeba marais wa wakati huo wa Rwanda na Burundi iliyokuwa inakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali. Tukio hilo lilitumiwa na Wahutu wenye misimamo mikali kama kisingizio cha kushambulia na kuua Watutsi.