Rais al Bashir: Sudan itauvuka mgogoro wa sasa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50531-rais_al_bashir_sudan_itauvuka_mgogoro_wa_sasa
Rais wa Sudan ameahidi kuwa nchi hiyo itaondokana na mgogoro unaosibu hivi sasa licha ya kuwepo pande zinazopambana na Sudan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 30, 2018 23:36 UTC
  • Rais al Bashir: Sudan itauvuka mgogoro wa sasa

Rais wa Sudan ameahidi kuwa nchi hiyo itaondokana na mgogoro unaosibu hivi sasa licha ya kuwepo pande zinazopambana na Sudan.

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa kwa kudhibiti hali ya kiuchumi nchi hiyo inaweza kuondokana na mgogoro wa sasa na kwamba kujiri wizi na uporaji kunaifanya haliya mambo kuwa mbaya zaidi na si suluhisho la matatizo. Ahmad Bela Waziri wa Mambo ya Ndani wa Sudan ametangaza uungaji mkono wake kwa Rais Omar al Bashir kutokana na maandamano yanayoendelea nchini humo na kueleza kuwa hawatatoa mwanya wa kutumiwa hali hiyo ya ghasia iliyopo sasa huko Sudan kuzusha mgawanyiko na ukosefu wa amani nchini humo. 

Wakati huo huo  Tayeb Babakar Ali Mkuu wa polisi ya Sudan ametangaza kuwa polisi itawasaka wahalifu wote ambao wamestafidi na maandamano yanayoendelea sasa nchini humo kufanya wizi na uporaji.  Maandamano ya mkate yalianza nchini Sudan tangu tarehe 19 mwezi huu kullamikia hali mbaya ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali khususan bei ya mkate na mafuta.