Omar al Bashir: Machafuko ya Sudan yanachochewa na baadhi ya makundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50745-omar_al_bashir_machafuko_ya_sudan_yanachochewa_na_baadhi_ya_makundi
Rais wa Sudan amewatuhumu watu aliowaita kuwa wanafanya njama kuwa wanahusika katika machafuko ya hivi sasa katika maandamano yanayofanyika nchini humo dhidi ya serikali yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 09, 2019 03:58 UTC
  • Rais Omar al Bashir wa Sudan
    Rais Omar al Bashir wa Sudan

Rais wa Sudan amewatuhumu watu aliowaita kuwa wanafanya njama kuwa wanahusika katika machafuko ya hivi sasa katika maandamano yanayofanyika nchini humo dhidi ya serikali yake.

Rais Omar al Bashir wa Sudan amesema kuwa wachochea ghasia hao walichoma moto makao makuu ya chama tawala katika moja ya maandamano nchini humo na kufanya hujuma na vitendo vya uharibifu. Rais wa Sudan ameyasema hayo pambizoni mwa mkutano wa jeshi uliofanyika mashariki mwa mji wa Atbara nchini humo.  Al Bashir ameongeza kuwa jeshi la Sudan litachukua hatua za kuilinda nchi na kukabiliana na njama zote za maadui. 

Makao makuu ya chama tawala cha Sudan yakiwaka moto

Rais wa Sudan ameyasema hayo  huku askari usalama wa nchi hiyo jana walikandamiza moja kati ya maandamano makubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini humo katika wiki za karibuni. Watu walioshuhudia wamesema kuwa, askari usalama wa Sudan walitumia gesi ya kutoa machozi kutanya mamia ya waandamanaji  katika mji wa El Gadarif mashariki mwa nchi hiyo. Maandamano ya mkate yalianza nchini Sudan Disemba 19 mwaka jana kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi.

Wafanya maandamano wanalalamikia kupanda kwa bei ya mkate na bidhaa nyingine muhimu na wanakosoa siasa za kiuchumi za serikali ya Omar al Bashir. Vilevile wanataka kuondoka madarakani kiongozi huyo.