Wasudani waandamana kupinga kuhukumiwa wafanya maandamano
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i51943-wasudani_waandamana_kupinga_kuhukumiwa_wafanya_maandamano
Maelfu ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo na katika miiji mingine kadhaa ya nchi hiyo wakitaka kuwa huru mahakama za nchi hiyo na kutowahukumu wafanya maandamano kwa mujibu wa sheria ya hali ya hatari.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 04, 2019 11:08 UTC
  • Wasudani waandamana kupinga kuhukumiwa wafanya maandamano

Maelfu ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo na katika miiji mingine kadhaa ya nchi hiyo wakitaka kuwa huru mahakama za nchi hiyo na kutowahukumu wafanya maandamano kwa mujibu wa sheria ya hali ya hatari.

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Sudan ambao wameandamana wakiitikia wito uliotolewa na Jumuiya ya wafanyakazi ya nchi hiyo na muungano wa wapinzani wamefanya maandamano na kutangaza kupinga kuhukumiwa wafanya maandamano kwa mujibu wa sheria ya hali ya hatari iliyotangazwa nchini humo hivi karibuni. Ripoti zinasema kuwa, askari usalama wa Sudan wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatanya waandamanaji huko Khartoum na katika miji mingine ya Sudan. 

Sudan ilianza kugubigwa na maandamano ya wananchi tangu Disemba 19 mwaka jana wanaolalamikia hali ngumu ya kiuchumi na kupanda bei za bidhaa muhimu khususan za mkate na petroli. 

Wafanya maandamano ambao wanataka Rais Omar al Bashir ang'atuke madarakani wametiwa mbaroni huku ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu ikieleza kuwa watu 44 wameuawa hadi sasa katika ghasia na machafuko huko Sudan.

Rais Omar al Bashir wa Sudan ambaye wananchi wanamtaka ang'atuke madarakani

Idara zinazosimamia hali ya hatari iliyotangazwa nchini Sudan pia Alhamisi iliyopita zilishughulikia kesi za watu wanane ambao walitiwa nguvuni kwa kushiriki maandamanono na kuwahukumu kifungo cha miaka sita hadi mitano jela.