Magaidi 13 wauawa katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini Misri
(last modified Tue, 29 Oct 2019 15:53:42 GMT )
Oct 29, 2019 15:53 UTC
  • Magaidi 13 wauawa katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini Misri

Maafisa wa serikali ya Misri wametangaza kuwa magaidi 13 wameuawa katika mapigano yaliyojiri baina yao na askari usalama katika mkoa wa Sinai Kaskazini nchini humo.

Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imesema kuwa, Shirika la Usalama wa Taifa limegundua makazi la magaidi hao katika eneo la al Arish mkoani Sinai Kaskazini na kuwaangamzia magaidi 13 katika operesheni iliyolenga eneo hilo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, askari usalama wa Misri pia wamekamata kiwango mikubwa cha silaha na zana za kivita yakiwemo mabomu na mikanda ya kujilipua katika maficho ya magaidi hao.

Misri imekuwa ikisumbuliwa na machafuko na mashambulizi ya hapa na pale hususan katika mkoa wa Sinai Kaskazini tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo mwaka 2013. 

Makundi ya kigaidi hususan lile linalojiita Wilaya ya Sinai yamukuwa yakifanya hujuma na mashambulizi ya mara kwa mara nchini Misri hususan katika mkoa wa Sinai Kaskazina. 

 

Tags