Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya Haftar dhidi ya raia huko Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i58192-umoja_wa_mataifa_walaani_mashambulizi_ya_haftar_dhidi_ya_raia_huko_libya
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametoa taarifa jana usiku akilaani mashambulizi ya anga yanayofanywa na kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya dhidi ya raia wa nchi hiyo chini ya uongozi wa Khalifa Haftar.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 30, 2019 03:14 UTC
  • Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya Haftar dhidi ya raia huko Libya

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametoa taarifa jana usiku akilaani mashambulizi ya anga yanayofanywa na kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya dhidi ya raia wa nchi hiyo chini ya uongozi wa Khalifa Haftar.

Ghasan Salame ametahadharisha kuwa mashambulizi dhidi ya raia si tu yanakiuka wazi wazi sheria za kimataifa bali yanatishia pia umoja na mshikamano huko Libya. Kundi la kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Kamanda Khalifa Haftar ambalo kwa miaka kadhaa sasa linadhibiti maeneo ya mashariki mwa Libya kwa kuungwa mkono na Saudi Arabia, Misri, Imarati na baadhi ya nchi za Magharibi lilisonga mbele katika miezi kadhaa ya karibuni kuelekea upande wa kaskazini mwa Libya.

Haftar mwezi Aprili mwaka huu aliwaamuru wanamgambo wake kuushambulia mji mkuu Tripoli; hatua iliyolaaniwa na jamii ya kimataifa. Watu zaidi ya 1090 wameuawa katika mji mkuu wa Libya Tripoli na wengine wasiopungua 5700 kujeruhiwa tangu kuanza mashambulizi hayo tajwa hadi hivi sasa.