Wapiganaji wa Haftar warejea nyuma kutoka mji wa Sirte nchini Libya
Askari wa serikali ya mwafaka wa kitaifa yenye makao yake magharibi mwa Libya wameelezea habari ya kukimbia wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar kutoka katika mji wa Sirte hadi umbali wa kati ya Tripoli na Bengazi.
Kukombolewa mji wa Sirte kumejiri baada ya kukombolewa na askari wa serikali ya mwafaka wa kitaifa miji miwili ya Bani Waled na Tarhunah. Kwa miaka kadhaa, mji wa Sirte umekuwa chini ya udhibiti wa wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) ambapo kundi hilo liliutangaza kuwa makao makuu yake ya ukhalifa kaskazini mwa Afrika. Hata hivyo kusonga mbele askari wa serikali ya mwafaka wa kitaifa kwenye mji mji huo, kuliuondoa mikononi mwa magaidi hao, huku wapiganaji wa Khalifa Haftar wakichukua tena udhibiti wake.
Mwenendo wa kusonga mbele jeshi la mwafaka wa kitaifa nchini Libya ulianza Alkhamisi iliyopita ulioenda sambamba na kukombolewa kikamilifu uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli. Wapiganaji wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya chini ya Khalifa Haftar walianzisha mashambulizi makali mwezi Aprili 2019 kwa lengo la kutaka kuudhibiti mji wa Tripoli. Hata hivyo muqawama wa wapiganaji wanaoiunga mkono serikali ya mwafaka wa kitaifa, umewafanya wapiganaji wa Haftar kurejea nyuma kutoka mji mkuu huo wa Libya, Tripoli.