Makumi ya wapiganaji wa Boko Haram wauliwa katika shambulizi la jeshi, Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61869-makumi_ya_wapiganaji_wa_boko_haram_wauliwa_katika_shambulizi_la_jeshi_nigeria
Makumi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la taifa la Nigeria dhidi ya ngome za kundi hilo huko kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 28, 2020 02:37 UTC
  • Makumi ya wapiganaji wa Boko Haram wauliwa katika shambulizi la jeshi, Nigeria

Makumi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la taifa la Nigeria dhidi ya ngome za kundi hilo huko kaskazini mwa nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria lilitangaza jana kwamba, wanajeshi wa nchi hiyo wameshambulia ngome ya kundi la Boko Haram katika maeneo mawili ya jimbo la Borno na kuua makumi ya wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi.

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilianzisha shughuli zake za kigaidi mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria na limepanua wigo wake hadi katika nchi za Niger, Cameroon na kaskazini mwa Chad.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, katika muongo mmoja wa shughuli za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamelazimishwa kuwa wakimbizi.

Serikali ya Nigeria inayoongozwa na Rais Muhamadu Buhari imeendelea kulaumiwa na kukosolewa kutokana na kuzembea katika kukakabiliana na kundi hilo la kigaidi ambalo limevuruga usalama wa nchi hiyo na nchi za jirani.