Waandamanaji wenye hasira nchini Afrika Kusini wachoma shule 13
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i6460-waandamanaji_wenye_hasira_nchini_afrika_kusini_wachoma_shule_13
Waandamanaji wenye hasira wameteketeza shule 13 katika mkoa wa kaskazini mwa Afrika Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 05, 2016 09:42 UTC
  • Waandamanaji wenye hasira nchini Afrika Kusini wachoma shule 13

Waandamanaji wenye hasira wameteketeza shule 13 katika mkoa wa kaskazini mwa Afrika Kusini.

Taarifa iliyotangazwa na jeshi la polisi imesema kuwa, hujuma hizo dhidi ya shule za serikali zilizoanza tangu siku ya Jumatatu iliyopita, zimejiri katika mkoa wa Limpopo, kaskazini mwa Afrika Kusini. Aidha polisi imesema kuwa, kufuatia vitendo hivyo, maelfu ya wanafunzi wamekosa kuendelea na masomo kutokana na shule zao kuteketezwa moto. Maandamano hayo yaliibuka kufuatia wakazi wa eneo moja mkoani hapo kupinga hatua ya viongozi wa Baraza Kuu la Manispaa ya mkoa huo ya kuyaingiza maeneo ya Vuwani na Livubu ndani ya manispaa mpya iliyoanzishwa hivi karibuni. Aidha waandamanaji wamepinga madai ya viongozi wa serikali ya eneo hilo kwamba, walichukua hatua hiyo kwa lengo la kuboresha huduma za kijamii na kusisitizia udharura wa maeneo hayo kuachwa katika manispaa ya Makhado kama ilivyokuwa tangu zamani. Kufuatia vurugu hizo, serikali ya mkoa wa Limpopo imeamua kufunga shule zingine zaidi ya 50. Mbali na shule, kadhalika ofisi za serikali na maduka nayo pia yamepigwa kufuli na serikali. Waziri wa Elimu nchini Afrika Kusini amesema, hatua ya waandamanaji kuchoma shule, imeathiri jitihada za serikali za kuboresha elimu katika mkoa huo.