Mwakilishi wa Umoja wa Afrika ziarani Misri kujadili bwawa la An Nahdhah
(last modified Tue, 02 Feb 2021 03:01:35 GMT )
Feb 02, 2021 03:01 UTC
  •  Mwakilishi wa Umoja wa Afrika ziarani Misri kujadili bwawa la An Nahdhah

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekutana na kufanya mashauriano na viongozi wa Misri huko Cairo kuhusu bwawa la An Nahdhah.

Bassam Razi Msemaji wa Rais wa Misri ameeleza kuwa, Moussa Faki Mahamat Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Abdelfattah al Sisi wa Misri na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Sami Shoukry kuhusu hitilafu zinazoendelea katika mvutano wa bwawa la An Nahdhah au Grand Renaissance Dam. 

Razi ameongeza kuwa,katika mazungumzo kati yake na Rais al Sisi na Sami Shoukry, Moussa Faki Mahamat ameshauriana na viongozi hao wa Misri kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kufanyika mwakani mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika,  masuala mengine muhimu ya nchi za Afrika kama vile ustawi wa kiuchumi, umoja wa kikanda, na amani na uthabiti.

Moussa Faki Mahamat katika mazungumzo na Sami Shoukry(kulia)

Wakati huo huo Rais al Sisi wa Misri ameeleza kuwa, kigezo na msimamo wa nchi yake kuhusu kikao cha Sudan,Misri na Ethiopia kuhusu bwawa la An Nahdhah chini ya usimami wa Umoja wa Afrika na kubainisha kuwa: nchi hizo tatu zinajifunga na hati ya kisheria ziliyosaini kuhusu ujenzi wa bwawa hilo. 

Rais wa Misri ameongeza kuwa, nchi yake haiafiki hatua yoyote inayoitia hatarini haki ya Misri katika Mto Nile. Ujenzi wa wa bwawa la An Nahdhah katika maji ya Mto Nile nchini Ethiopia umeibua mzozo na mvutano mkubwa wa kugombea maji kati ya nchi tatu za Misri, Ethiopia na Sudan tangu mwaka 2011. Misri na Sudan kwa upande wake zinasema kuwa, zina wasiwasi kuwa mgawo wa maji kwa kila mmoja ya nchi hizo utapungua iwapo maji yatapunguzwa katika bwawa hilo. 

Kupunguzwa majiya bwawa la An Nahdhah ni tishio kubwa khususan kwa Misri; kwa sababu karibu asilimia 90 ya maji inayohitajia nchi hiyo hujidhaminia kutoka Mto Nile.   

Tags