Afrika Kusini: Chanjo ya corona ya AstraZeneca inavunja moyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i66956-afrika_kusini_chanjo_ya_corona_ya_astrazeneca_inavunja_moyo
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini amesema amevunjwa moyo na taathira ndogo ya chanjo ya corona ya AstraZeneca kwa virusi vipya vya corona.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 17, 2021 07:13 UTC
  • Afrika Kusini: Chanjo ya corona ya AstraZeneca inavunja moyo

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini amesema amevunjwa moyo na taathira ndogo ya chanjo ya corona ya AstraZeneca kwa virusi vipya vya corona.

Baada ya matokeo ya kuvunja moyo ya chanjo ya corona ya Uingereza ya AstraZeneca katika kukabiliana na aina mpya ya virusi vya Covid-19 vinavyoendelea kusambaa kwa wingi katika nchi za Uingereza na Afrika Kusini, Pretoria imesema chanjo iliyonunuliwa kutoka Uingereza inapaswa kutumwa katika nchi nyingine. 

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Zweli Mkhize amesema kuwa serikali ya nchi hiyo imetoa pendekezo la kupelekwa chanjo ya AstraZeneca iliyokuwa imenunulwia na nchi hiyo katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ambazo hazijakumbwa na aina mpya ya virusi vya corona.

Zweli Mkhize ameongeza kuwa, habari zinazosema kuwa chanjo ya AstraZeneca haina taathira kwa virusi vipya vya corona inavunja moyo na sasa shehena ya chanjo hiyo iliyonunuliwa na Pretoria kutoka Uingereza itauzwa kwa nchi nyingine. 

Wataalamu wameng'amua kuwa baada ya kufanyiwa majaribio kwa watu 2026, chanjo ya corona ya AstraZeneca haina taathira ya maana kwa aina mpya ya virusi vya corona kama vile vya Afrika Kusini. 

Chanjo ya corona

Aina hiyo mpya ya virusi vya corona ina nguvu kubwa zaidi ya maambukizi japokuwa hadi sasa haijathibitika kuwa vinaua zaidi kuliko virusi asili vya corona.