Ramaphosa: Desmond Tutu alikuwa mzalendo asiye na kifani
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter, Rais wa Afrika Kusini amemtaja Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwanaharakati wa vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo, kuwa alikuwa mzalendo wa kipekee.
Cyril Ramafosa meandika kuwa: “Kifo cha Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwanaharakati katika vuguvugu la kupinga ubaguzi wa rangi, kimewafanya watu wa Afrika Kusini waagane na mwanachama mwingine wa kizazi cha aina yake kilichoitunuku uhuru Afrika Kusini."
Rais wa Afrika Kusini amemuombea msamaha na maghufira Desmond Tutu na kuandika: "Roho yake itaendelea kuangalia kulinda mustakabali wa taifa la nchi hii."
Askofu Mkuu mstaafu Desmond Tutu, ambaye ni nembo ya harakati za kupiga vita mfumo wa ubaguzi wa rangi wa Apartheid nchini Afrika Kusini, alifariki dunia jana akiwa na umri wa miaka 90.
Miaka kadhaa kabla ya kusambaratika utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, Tutu aliwaandikia barua viongozi wawili wa utawala huo, John Vorster na P.W. Botha, akionya kwamba Afrika Kusini itakumbwa na machafuko makubwa iwapo utawala wa ubaguzi wa rangi, Apartheid hautavunjwa.
Kwa miaka mingi, Desmond Tutu alikuwa rafiki na mwenza wa Nelson Mandela, shujaa wa uhuru wa Afrika Kuisini na rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo.