Wanajeshi wa serikali wakomboa maeneo muhimu ya mji wa Sirte Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i8875-wanajeshi_wa_serikali_wakomboa_maeneo_muhimu_ya_mji_wa_sirte_libya
Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo televisheni ya Russia Today vimeripoti habari ya kukombolewa kikamilifu fukwe za mji wa Sirte na maeneo mengine muhimu ya mji huo wa baada ya kundi la Daesh kuufanya mji huo kuwa ngome yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2016 02:53 UTC
  • Wanajeshi wa serikali wakomboa maeneo muhimu ya mji wa Sirte Libya

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo televisheni ya Russia Today vimeripoti habari ya kukombolewa kikamilifu fukwe za mji wa Sirte na maeneo mengine muhimu ya mji huo wa baada ya kundi la Daesh kuufanya mji huo kuwa ngome yake.

Mohamed al-Gasri, msemaji wa vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amesema kuwa, jana askari wa nchi hiyo waliingia mjini Sirte na kufika hadi katikati ya mji huo. Amesema mapigano yanaendelea kati ya askari wa serikali na wanamgambo wa Daesh.

Ameongeza kuwa, operesheni hiyo haitachukua muda mrefu na kwamba ni matarajio yake kuwa mji wa Sirte utakombolewa kikamilifu katika kipindi cha siku mbili au tatu zijazo.

Amesema, wasiwasi wao pekee ni wanamgambo wa ISIS wanaopiga risasi kutokea mbali, na hilo ni tatizo kwa vita vya ndani ya mji ambapo jeshi la serikali linafikiria pia usalama wa raia.

Taarifa zinasema kuwa, maeneo kadhaa muhimu sana katika viunga vya mji wa Sirte kama vile uwanja mmoja wa ndege, vituo kadhaa vya kijeshi na barabara moja kuu yamekombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.