Dunia yaipongeza Kenya kwa kupunguza uharamia Afrika Mashariki
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i9493-dunia_yaipongeza_kenya_kwa_kupunguza_uharamia_afrika_mashariki
Hatua ya Kenya kutuma jeshi lake nchini Somalia imechangia kupunguza kwa kiasi kikubwa uharamia katika pwani ya Bahari ya Hindi Afrika Mashariki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 18, 2016 09:25 UTC
  • Dunia yaipongeza Kenya kwa kupunguza uharamia Afrika Mashariki

Hatua ya Kenya kutuma jeshi lake nchini Somalia imechangia kupunguza kwa kiasi kikubwa uharamia katika pwani ya Bahari ya Hindi Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Maaifa la Kukabiliana na Uharama katika Pwani ya Somalia (CGPCS), kuwepo wanajeshi wa Kenya Somalia kumetoa mchango mkubwa katika vita dhidi ya ugaidi.

Ripoti hiyo imetolewa katika kikao cha 19 cha CGPCS huko Ushelisheli ambapo nchi wanachama zimetakiwa kubadilishana habari na kushirikiana na wakuu wa Somalia ili kuwatia mbaroni na kuwafikisha kizimbani vinara wa uharamia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Uharamia katika Pwani ya Somalia liliundwa mwaka 2009 kufuatia azimio la Baraza la Usalama. Shirika hilo huleta pamoja nchi, mashirika na makundi yanayohusika katika vita dhidi ya uharamia.

Kenya ilituma askari wake Somalia Oktoba mwaka 2011 kukabiliana na magaidi wa kundi la Al Shabab ambao walikuwa wakitekeleza hujuma na kuwateka nyara watalii ndani ya nchi hiyo.