Maonyesho ya Qur'ani Tukufu yaanza Senegal
Maonyesho makubwa ya Qur'ani Tukufu yameanza Dakar, mji mkuu wa Senegal huko Magharibi mwa Afrika kwa hima na juhudi za Chuo Kikuu cha Al-Mustafa.
Hossein Asadi, mkurugenzi wa ofisi ya mwakilishi wa kikanda wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa nchini Senegal, amesema kuwa chuo hicho kina nafasi muhimu sana katika upanuzi wa shughuli za Qur'ani katika uwanja wa kimataifa na kuongeza kuwa: Kutarjumu Qur'ani Tukufu katika lugha za wenyeji za Senegal ni mojawapo ya kazi za hivi karibuni za ofisi ya Chuo Kikuu cha al-Mustafa nchini Senegal.
Mkurugenzi wa ofisi ya mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa nchini Senegal ameongeza kuwa: Maonyesho makubwa ya Qur'ani Tukufu ambayo yameanza leo (Jumamosi) kwa muda wa wiki moja katika mji mkuu wa Senegal na ushirikiano wa jumuiya za Qur'ani nchini humo na Chuo Kikuu cha Mustafa, ni tukio muhimu katika uwanja wa kustawisha elimu na mafunzo ya Qur'ani Tukufu.
Chuo Kikuu cha Al-Mustafi Al-Alamiya ni taasisi ya kisayansi na kimataifa yenye mfungamo na wa Chuo Kikuu cha Kidini cha Qum nchini Iran. Lengo kuu la chuo hicho ni kupanua sayansi ya Kiislamu, kibinadamu na kijamii, kwa njia ya elimu, utafiti na malezi na kinatoa elimu na mafunzo kwa idadi kubwa ya watu duniani kote.