-
Waasi wa M23 wateka vijiji viwili Kongo na kuhatarisha makubaliano ya Doha
Jul 30, 2025 04:20Waasi wa M23 wameteka vijiji viwili katika eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, licha ya makubaliano ya amani waliyosainiwa hivi karibuni huko Qatar.
-
Watekaji nyara nchini Nigeria wamewaua mateka 35 licha ya kupokea mlungura
Jul 29, 2025 23:43Ripoti kutoka Nigeria zinasema kuwa, maafa mengine yamejiri kaskazini magharibi mwa nchi hiyo baada ya majambazi katika Jimbo la Zamfara kuwaua watu 33 waliowateka nyara mwezi Februari mwaka huu licha ya kupokea pesa ya kikomboleo au mlungura wa zaidi ya dola 33,000.
-
4 wauawa, mamia watiwa nguvuni katika maaandamano ya kupinga kupanda bei ya mafuta huko Angola
Jul 29, 2025 23:14Watu wasiopungua wanne wamepoteza maisha na mamia ya wengine kutiwa nguvuni katika maandamano ya ghasia huko Angola kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta.
-
Harakati za Ukombozi Afrika: Magharibi inajaribu tena kugawanya na kutawala Afrika
Jul 29, 2025 08:00Harakati za ukombozi kutoka nchi sita za Afrika zimekutana mjini Johannesburg, Afrika Kusini, kwa lengo la kuimarisha mshikamano dhidi ya kuingiliwa kwa masuala ya bara hili na mataifa ya Magharibi. Washiriki wameonya kuwa nguvu za kigeni zinajaribu kuligawanya tena Bara la Afrika na kulitawala kiuchumi kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
-
Serikali ya Algeria yafuta Hadhi Maalum kwa Ubalozi wa Ufaransa
Jul 29, 2025 07:47Algeria imefuta kadi zote za hadhi maalumu zilizokuwa zimetolewa kwa wafanyakazi wa Ubalozi wa Ufaransa katika bandari na viwanja vya ndege vya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya kile ambacho Algiers inasema ni vikwazo vilivyowekwa kwa wanadiplomasia wake nchini Ufaransa.
-
Nchi za Karibiani zawania kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika
Jul 29, 2025 07:39Nchi za Jumuiya ya Karibiani (CARICOM) zinawania kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika, huku taswira ya biashara ya kimataifa ikibadilika kwa kasi.
-
Kwa nini serikali ya Sudan inachukulia uundaji wa serikali hasimu kuwa tishio kubwa?
Jul 29, 2025 07:26Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imelaani vikali tangazo la kuundwa serikali hasimu na Vikosi vya Msaada wa Haraka vinavyoongozwa na "Mohammed Hamdan Dagalo", anayejulikana kwa jina la "Hemedti".
-
UN na nchi za Afrika zakutana Ethiopia kutathmini hali ya mabadiliko ya mifumo ya chakula duniani
Jul 29, 2025 03:30Umoia wa Mataifa, na nchi za Afrika zimekutana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kutathmini hali ya mabadiliko ya mifumo ya chakula iliyosababishwa na migogoro ya vita katika maeneo kadhaa duniani.
-
Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya watu zaidi ya 40 Ituri DRC
Jul 28, 2025 23:11Ujumbe wa Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umelaani vikali shambulio lililotokea Ituri na kupelekea makumi ya watu kuuawa.
-
Waasi wa ADF waua raia takriban 43 katika shambulio la usiku Ituri, DRC
Jul 28, 2025 09:40Takriban raia 43 wamepoteza maisha katika shambulio la usiku lililotokea jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), tukio linaloaminika kutekelezwa na waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces (ADF), kinachodaiwa kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Daesh tawi la kati mwa Afrika.