-
Abiy Ahmed atangaza kukamilika Bwawa la Renaissance, azialika Misri na Sudan katika sherehe za ufunguzi
Jul 03, 2025 23:41Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ametangaza "kukamilika kazi" katika mradi wa Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) kwenye Mto Nile, akisema litazinduliwa mwezi Septemba. Vilevile ametoa wito kwa Misri, Sudan, na watu wa Bonde la Mto Nile kuungana katika kusherehekea "hatua hiyo ya kihistoria."
-
Chama cha siasa cha '47 Voices of Kenya Congress', chaingia rasmi kwenye uwanja wa siasa
Jul 03, 2025 08:34Chama kipya cha kisiasa kinachoongozwa na vijana kilichopewa jina ‘47 Voices of Kenya Congress', kimeingia rasmi kwenye uwanja wa siasa nchini humo. Hali hiyo inapelekea kuujitokeza sura mpya katika siasa za vijana wa Kenya maarufu kama Gen Z.
-
Jeshi la Mali: Zaidi ya magaidi 80 wauawa katika mashambulizi yaliyoratibiwa nchini humo
Jul 03, 2025 00:30Magaidi zaidi ya 80 wameuawa katika mashambulizi yaliyolenga maeneo kadhaa ya katikati na magharibi mwa Mali.
-
Helikopta ya walinda amani wa Umoja wa Afrika yaanguka Somalia
Jul 02, 2025 08:38Helikopta ya Kikosi cha Usaidizi na Uimarishaji Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AUSOM) imeanguka leo Jumatano katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.
-
WFP: Mamilioni ya raia wa Sudan wanakabiliwa na janga la njaa
Jul 01, 2025 23:10Mamilioni ya wakimbizi wa Sudan wanakabiliwa na janga la njaa huku uhaba mkubwa wa fedha ukilazimisha Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kupunguza msaada muhimu unaoweza kuokoa maisha ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo.
-
Rais wa Kongo DR ataka haki itendeke mkabala wa jinai zilizotekelezwa mashariki mwa nchi hiyo
Jul 01, 2025 08:56Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameeleza kuwa serikali yake itaendelea kuwa imara katika kudai haki za wahanga wa jinai zilizofanywa mashariki mwa nchi hiyo, licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini hivi karibuni kati ya nchi hiyo na Rwanda.
-
Kiongozi wa upinzani anayezuiliwa Chad akomesha mgomo wa kula
Jul 01, 2025 03:29Kiongozi wa upinzani nchini Chad aliyewahi kuwa waziri mkuu, Succes Masra, amekomesha mgomo wa kula baada ya takriban wiki moja.
-
Gachagua aonywa huwenda akashtakiwa ikibainika alihusika na ghasia za maandamano
Jul 01, 2025 03:27Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua atakamatwa na kushtakiwa kama Mkenya mwengine yeyote iwapo ushahidi utamhusisha na ghasia zilizoshuhudiwa nchini humo mnamo Juni 25. Hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi ya Kenya (DCI).
-
Jeshi la Somalia laua zaidi ya magaidi 37 wa al-Shabaab
Jun 30, 2025 08:00Kikosi maalum cha Danab cha Jeshi la Somalia kimewaua zaidi ya wanamgambo 37 wa kundi la al-Shabaab katika kijiji cha Maqooqaha, kilichoko magharibi mwa Buulo Xaaji katika eneo la Lower Jubba, kusini mwa nchi.
-
Watoto zaidi ya 239 wafariki magharibi mwa Sudan kwa njaa na ukosefu wa dawa
Jun 30, 2025 07:52Watoto wasiopungua 239 wamefariki dunia katika eneo la magharibi mwa Sudan tangu Januari mwaka huu kutokana na ukosefu wa chakula na dawa, kwa mujibu wa taarifa ya Mtandao wa Madaktari wa Sudan iliyotolewa Jumapili.