-
Wamorocco: Mgogoro wa kibinadamu Gaza unatisha
May 12, 2025 07:42Wananchi wa Morocco wameandamana kuunga mkono Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza, wakitangaza mshikamano wao na watoto wa eneo hilo la Palestina lililozingirwa ambao wanakabiliwa na njaa, kiu na maradhi; huku mgogoro mbaya wa kibinadamu uliosababishwa na Wazayuni ukiendelea kuwasakama.
-
Makumi wauawa katika mashambulizi ya wabeba silaha Benue, Nigeria
May 12, 2025 07:40Takriban watu 23 waliuawa huku wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi ya watu waliojizatiti kwa silaha katika Jimbo la Benue nchini Nigeria.
-
Watu wasiojulikana waua watu 12 na kujeruhi 17 Sudan Kusini
May 12, 2025 02:14Kundi la watu wasiojulikana wenye silaha wameua takriban watu 12 na kujeruhi wengine 17 huko Sudan Kusini mapema jana Jumapili.
-
Algeria yawafukuza majajusi 2 wa Ufaransa kwa kuingia nchini na pasi za bandia za kusafiria
May 11, 2025 22:32Serikali ya Algeria imewafukuza maajenti wawili wa ujasusi wa Ufaransa kwa kuingia nchini humo kwa kutumia "pasi bandia za kidiplomasia " ikiwa ni ishara mpya ya kuongezeka mvutano kati ya nchi mbili hizo.
-
Ethiopia yaunda polisi wa baharini kulinda Bwawa la Renaissance
May 11, 2025 22:32Ethiopia imetangaza kuunda kikosi kipya cha polisi wa baharini kitakachokuwa na jukumu la kuhakikisha usalama karibu na Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD).
-
Benin yarejesha kiti cha kifalme kilichoporwa na wazungu wakati wa utawala wa kikoloni
May 11, 2025 22:31Wizara ya Utalii, Utamaduni na Sanaa ya Benin imetangaza kwamba kitu cha nadra cha kifalme kinachoitwa "Katakli" kitarejeshwa rasmi nchini humo kutoka Finland, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni zaidi katika juhudi zinazoendelea kufanywa na Benin kurejesha urithi wake wa kitamaduni ulioporwa na wakoloni wa Ulaya.
-
Waliokufa kwenye mafuriko DRC wafika 62 na 50 hawajulikani walipo
May 11, 2025 08:36Takriban watu 62 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine 50 hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa kuvikumba vijiji vilivyoko karibu na Ziwa Tanganyika katika jimbo la Kivu Kusini, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Watu 33 wauawa katika mashambulizi yanayoshukiwa kuwa ya RSF nchini Sudan
May 11, 2025 08:34Takriban watu 33 wameuawa nchini Sudan katika mashambulio yanayoshukiwa kufanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huku vita vya kikatili vya miaka miwili vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi vikiendelea kuchukuka roho za watu na kuinakamisha Sudan.
-
Utafiti: Lishe za magharibi zinawadhuru Waafrika
May 11, 2025 05:43Utafiti wa hivi karibuni uliofanyika umebainisha kwa mara ya kwanza kwamba Waafrika wanaokumbatia lishe za Kimagharibi zenye vyakula vilivyosindikwa kwa wingi, sukari na mafuta, wanakabiliwa na kuongezeka kwa uvimbe mwilini (Inflammation), kinga dhaifu, na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
-
Charles Hillary, aliyewahi kuwa mtangazaji mahiri afariki dunia
May 11, 2025 01:03Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, amefariki dunia alfajiri ya leo Mei 11, 2025.