-
Misri yapinga madai ya Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza
Apr 19, 2025 02:42Jumuiya ya Wahandishi wa Misri imepinga madai ya Marekani kuhusu Ukanda wa Gaza
-
Wananchi wa Morocco wafanya maandamano 105 kuiunga mkono Gaza
Apr 19, 2025 02:35Televisheni ya al Jazeera yenye makao yake nchini Qatar imetangaza kuwa wananchi wa Morocco wamefanya maandamano 105 katika miji 58 ya nchi hiyo wakitangaza mshikamano wao na kuwaunga mkono watu madhulumu wa Ukanda wa Gaza na kulaani vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.
-
Mjukuu wa Houphouët-Boigny apasishwa na upinzani kugombea kiti cha rais Ivory Coast
Apr 18, 2025 22:52Katika hatua muhimu kwenye siasa za Ivory Coast, Chama cha Kidemokrasia cha Côte d'Ivoire (PDCI), moja ya vyama maarufu vya upinzani, kimempasisha mwenyekiti wake, Tidjane Thiam, kugombea katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Oktoba 25, 2025.
-
UN yalaani mashambulizi ya RSF huko El Fasher, yatoa wito wa kuondolewa mzingiro
Apr 18, 2025 10:46Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi "ya mara kwa mara" ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan, likitaka kukomeshwa mzingiro wa mji huo.
-
Mawaziri wa Afya wa Afrika wazindua kampeni ya chanjo ya Polio katika eneo la Bonde la Ziwa Chad
Apr 18, 2025 10:45Mawaziri wa afya wa Afrika kutoka eneo la Bonde la Ziwa Chad wamezindua kampeni ya chanjo yenye lengo la kuwalinda watoto milioni 83 walio chini ya umri wa miaka 5 dhidi ya aina ya pili ya ugonjwa wa Polio.
-
Uganda inapanga sheria kuruhusu mahakama ya kijeshi kuwahukumu raia
Apr 18, 2025 10:12Serikali ya Uganda inakusudia kuanzisha sheria ya kuruhusu mahakama za kijeshi kuwahukumu raia kwa baadhi ya makosa hata baada ya jambo hilo kupigwa marufuku na Mahakama ya Juu.
-
Mamia hawajapatikana baada ya boti kuteketea moto, kuzama DRC
Apr 18, 2025 03:24Mamia wa watu wangali hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa na mamia ya abiria kuzama baada ya kuwaka moto katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua watu zaidi ya 50.
-
Sudan imeingia mwaka wa tatu wa vita; wachezaji wa kikanda wana nafasi gani?
Apr 17, 2025 23:03Wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vikiingia katika mwaka wake wa tatu, mapigano, kuhama makazi na njaa vimeifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi zilizotumbukia kwenye mgogoro mkubwa zaidi duniani.
-
Jeshi la Sudan: Raia wasiopungua 62 wameuawa katika shambulio la RSF jimboni Darfur
Apr 17, 2025 10:25Jeshi la Sudan leo Alhamisi limetangaza kuwa raia wa nchi hiyo wasiopungua 62 wameuawa katika shambulio la makombora la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mji wa al Fasher ambao ni makao makuu ya jimbo la Darfur ya Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Watu kadhaa wajeruhiwa katika maandamano ya kulalamikia kuaga dunia wanafunzi 3 Tunisia
Apr 17, 2025 10:19Watu kadhaa wamejeruhiwa katika maandamano yaliyofanyika katika mji wa Mezzouna katikati mwa Tunisia kufuatia vifo vya wanafunzi watatu. Wanafunzo hao wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa shule.