-
Nigeria: Karibu wapiganaji 10,000 wa zamani wa Boko Haram waunganishwa katika jamii
Jun 16, 2026 11:00Mamlaka husika katika Jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria zimearifu kuwa karibu wapiganaji 10,000 wa zamani wa kundi la waamgambo wa Boko Haram sasa wameunganishwa tena katika jamii chini ya mpango unaofadhiliwa na serikali wa kurekebisha tabia na kuhimiza kuachana na makundi ya uasi.
-
Serikali ya Afrika Kusini yasema imewarejesha nyumbani wageni 2,745 ndani ya wiki moja
Jun 15, 2026 12:20Afrika Kusini imewarejesha nyumbani wageni 2,745 katika wiki moja baada ya Rais Cyril Ramaphosa kuapa kuchukua hatua kali dhidi ya uhamiaji haramu.
-
Sudan: RSF inafanya biashara haramu ya viungo vya binadamu
Jun 15, 2026 04:24Serikali ya Sudan imelituhumu kundi la Rapid Support Forces (RSF) kuwa linaendesha mtandao wa biashara haramu ya viungo vya binadamu ndani ya magereza ya Daqris na Shala huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini, ambalo kwa mujibu wa makadirio ya serikali ya Khartoum, lina wafungwa karibu 20,000 wa kijeshi na raia.
-
Jenerali mstaafu Nigeria afariki akiwa ametekwa, rais aapa kuchukua hatua kali
Jun 14, 2026 11:59Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, ameapa kuangamiza wale aliowataja kuwa ni “maadui wakubwa” wa nchi hiyo baada ya jenerali mstaafu wa jeshi kufariki dunia akiwa mikononi mwa watekaji nyara.
-
Maambukizi ya Ebola DRC yafikia 710 huku hofu ikitanda
Jun 14, 2026 11:57Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefikia 710, wakiwemo watu 149 waliofariki dunia, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi na Wizara ya Afya ya nchi hiyo.
-
Idadi kubwa ya walioambukizwa Ebola DRC na Uganda ni wanawake na wasichana
Jun 14, 2026 03:09Wanawake na wasichana wanawakilisha asilimia 53.4 ya wagonjwa wa Ebola waliothibitishwa kwa vipimo vya maabara katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Uganda, sawa na wagonjwa 244 kati ya 457 kwa mujibu wa taarifa za wagonjwa katika maeneo zilikopatikana. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake.
-
Rais wa Somalia aituhumu Israel kwa kutumia mzozo kati ya Somalia na Somaliland kwa maslahi yake
Jun 13, 2026 11:16Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud leo amelaani hatua ya Israel ya kuitambua rasmi Somaliland, na kuituhumu Tel Aviv kuwa inatumia mzozo kati ya Mogadishu na eneo hilo lililojitenga na Somalia kwa maslahi yake.
-
WHO: Ebola inaenea katika maeneo mapya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Jun 13, 2026 02:37Shirika la Afya Duniani (WHO) jana Ijumaa lilitangaza kuwa mlipuko wa Ebola kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo sasa unaenea katika maeneo mapya.
-
Rais wa Nigeria atangaza mauaji ya wapiganaji 13,000 mwaka jana
Jun 12, 2026 12:36Rais wa Nigeria, Bola Ahmed Tinubu, ametangaza leo Ijumaa kwamba "magaidi" wasiopungua 13,000 waliuawa nchini Nigeria mwaka jana, akisisitiza kwamba idadi ya vifo vinavyotokana na uasi wa kutumia silaha nchini humo imepungua kwa 81% tangu alipochukua madaraka Mei 2023.
-
Ujenzi wa kituo cha Ebola cha Marekani nchini Kenya unaendelea kwa kasi
Jun 12, 2026 04:38Licha ya amri ya Mahakama Kuu ya Kenya ya kusimamisha ujenzi wa kituo cha karantini cha kuwapokea raia wa Marekani wanaoshukiwa kuwa na Ebola na maandamano ya Wakenya wenye hasira huko Nanyuki, ujenzi wa kituo hicho unaendelea kwa kasi ndani ya kambi ya jeshi ya Laikipia katikati mwa Kenya.