-
Somalia yafuta mikataba yote iliyosainiwa na UAE
Jan 13, 2026 02:33Somalia imeamua kufuta makubaliano yote yaliyosainiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, ili kukabiliana na hatua za Abu Dhabi zinazodhoofisha mamlaka, umoja na uhuru wa nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza la Mawaziri la Somalia.
-
RSF yaua watu 27 huko Sennar, mashariki mwa Sudan
Jan 13, 2026 02:10Watu 27 wameuawa na wengine 13 kujeruhiwa katika shambulio la wapiganaji wa Rapid Support Forces lililolenga mji wa Sinja, wakati watu waliokimbia makazi yao kutoka Darfur Kaskazini wakiendelea kuongezeka, huku Jeshi la Sudan likitangaza mauaji ya mamia ya wanachama wa RSF katika maeneo tofauti.
-
Ghana imelipa deni la dola bilioni 1.47 la sekta ya nishati
Jan 13, 2026 00:13Ghana imelipa jumla ya dola za Marekani bilioni 1.47 mwaka 2025 ili kufuta madeni ya muda mrefu ya sekta ya nishati na kurejesha dhamana ya Benki ya Dunia kwa sekta hiyo. HIi ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Wizara ya Fedha ya nchi hiyo.
-
Kwa nini Misri inapinga kuhamishwa kwa nguvu Wapalestina hadi Somaliland?
Jan 13, 2026 00:10Misri imetangaza kupinga vikali kuhamishwa kwa lazima kwa Wapalestina hadi Somaliland eneo lililotangaza kujitenga na Somalia.
-
Waliuliwa huku wakisoma Qur'ani: Simulizi ya kusikitisha ya mauaji ya RSF huko Darfur
Jan 11, 2026 23:44Ushahidi uliotolewa na manusura wa mauaji ya kupanga na kampeni za mauaji ya halaiki na ya kikabila, hasa dhidi ya kabila la "Masalit", yaliyofanywa na wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) katika eneo la Darfur, umefichua picha ya kutisha ya hali ya kibinadamu katika eneo hilo, kwani athari zake haziishii tu kwenye majeraha ya vita, bali zimegeuka kuwa mauaji ya halaiki.
-
Serikali ya Sudan yarudi Khartoum baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita
Jan 11, 2026 23:44Baada ya zaidi ya miaka miwili ya mapigano makali kati ya jeshi la taifa na wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), serikali ya Sudan imerejea rasmi mjini Khartoum, hatua ambayo Waziri Mkuu Kamel Idris aliitaja kuwa “mgeuko muhimu katika safari ya taifa.”
-
OIC imefanya kikao kujadili kadhia ya Somaliland, baada ya Wazayuni kuitambua rasmi
Jan 11, 2026 07:27Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitisha kikao mjini Jeddah, Saudi Arabia kujadili kadhia ya Somaliland na hasa baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutambua rasmi kujitenga na ardhi nyingine za Somalia.
-
Afrika Kusini yatetea mazoezi ya kijeshi ya BRICS
Jan 11, 2026 07:27Serikali ya Afrika Kusini imetetea mazoezi ya kijeshi ya wiki moja yanayozishirikisha nchi kubwa za Russia, Iran, China na nchi nyingine muhimu, ikisema kuwa maneva hayo kwenye pwani yake ni majibu muhimu ya kuzuia kuongezeka mivutano ya baharini ulimwenguni.
-
Somalia: Israel kuwahamishia kwa nguvu Wapalestina Somaliland ni kinyume cha sheria za kimataifa
Jan 11, 2026 03:26Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Ahmed Moalim Fiqi, ameishutumu Israel kwa kupanga kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika eneo lililojitenga la Somaliland, akiukashifu mpango huo alioutaja kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa sheria za kimataifa.
-
Ethiopia yaanza ujenzi wa 'uwanja mkubwa zaidi wa ndege barani Afrika'
Jan 11, 2026 03:03Ethiopia imezindua ujenzi wa 'uwanja mkubwa zaidi wa ndege barani Afrika' utakaogharimu dola bilioni 12.5 za Marekani.