IRGC: Tumelenga moyo wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa makombora ya balestiki + Picha
(last modified 2024-10-02T03:12:00+00:00 )
Oct 02, 2024 03:12 UTC
  • IRGC: Tumelenga moyo wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa makombora ya balestiki + Picha

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuwa makumi ya makombora ya balistiki yametumika kulenga moyo wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina (Israel).

Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu inasema: Baada ya muda wa kujizuia mbele ya ukiukwaji wa mamlaka ya kujitawala ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Mujahid Ismail Haniyeh, na kwa mujibu wa haki ya nchi ya kujilinda chini ya Hati ya Umoja wa Mataifa, na kutokana na kushadidi maovu ya utawala huo ghasibu ukiungaji mkono na Marekani katika mauaji ya halaiki ya wananchi wa Lebanon na Gaza na kumua shahidi Mujahid mkubwa, kiongozi wa Mhimili wa Muqawama na Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, na kuuawa shahidi Kamanda na mshauri wa ngazi ya juu wa IRGC huko Lebanon, Meja Jenerali Abbas Nilforoushan, Kikosi cha Anga cha IRGC kumepiga maeneo muhimu ya kijeshi na kiusalama katika moyo wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina (Israel).

Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeongeza kuwa: Iwapo utawala wa Kizayuni utachukua hatua za kijeshi baada ya operesheni hiyo ambayo imefanyika kwa mujibu wa haki za kisheria za nchi na sheria za kimataifa, itakabiliwa na mashambulizi shadidi na yenye uharibifu mkubwa zaidi.

Ving'ora vilisikika katika maeneo yote ya Israel jana Jumanne usiku wakati Iran ilipofurumusha mamia ya makombora dhidi ya utawala huo, katika shambulio la kulipiza kisasi lililopewa jina la Operesheni Ahadi ya Kweli -2 (Operesheni True Promise II).

Tel Aviv

Miale na makombora vilionekana katika anga ya Tel Aviv na milipuko ilisikika katika eneo la al-Quds inayokaliwa kwa mabavu na kuwafanya walowezi wa Kizayuni wakimbilie mafichoni.

Gazeti la Israel la Haaretz limeripoti kuwa, "vipigo vya moja kwa moja" huko Negev, Sharon na maeneo mengine kutokana na shambulio la Iran.

Mashambulizi ya Iran ambayo kwa mujibu wa duru mbalimbali za habari yameharibu kabisa kambi ya Jeshi la Anga la Israel ya Nevatim huko Neveg, yameibua sherehe na vifijo katika nchi mbalimbali hususan huko Palestina na Lebanon. 

Hapa chini tumeweka baadhi ya picha kuhusu mashambulizi hayo.

Athari za vipigo vya makombora ya Iran dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni
Mtumiaji wa mitandao ya kijamii akifurahia vipigo vya makombora vilivyotolewa na Iran dhidi ya Israel
Kombora la Iran likiielekea kwenye maeneo ya utawala wa Kikzayuni
Mashambulizi ya Iran dhidi ya Israel yameleta faraja kubwa kwa wapenda haki duniani

 

Tags