Dec 03, 2023 03:15 UTC
  • Kan'ani Chafi: Mashambulio mapya dhidi ya Gaza ni kashfa kubwa ya kimaadili kwa Marekani

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameandika katika kujibu idhini ya Marekani kwa mashambulizi mapya yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza kwamba, hii ni kashfa kubwa ya kimaadili kwa serikali ya Marekani na imeonyesha sura halisi ya haki za binadamu ya Washington kwa walimwengu.

Nasser Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran, akitoa radiamali yake kwa duru mpya ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuuawa shahidi Wapalestina zaidi ya 200, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X: Takribani mashahidi 200 na majeruhi 600 ni matokeo ya mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa muda wa saa 24.

Aidha ameanduika, baada ya hatua ya utawala huo kuhitimisha usitishaji vita wa siku 7, mashambulizi hayo yameanza tena idhini na baraka za Marekani na kuongeza orodha nyingine ndefu ya uhalifu wa kivita, mauaji ya watoto wachanga na mauaji ya halaiki kwa uhalifu wa kutisha wa kuua zaidi ya Wapalestina 16,000 ndani ya siku 48.

 

Msemaji wa taasisi ya kidiplomasia ya Iran ameongeza kuwa: Baada ya kuwaua zaidi ya Wapalestina elfu 15, wavamizi wa Kizayuni wameanza duru mpya ya mauaji katika kivuli cha kuendelea uungaji mkono wa serikali ya Marekani. Mataifa na aghalabu ya tawala za dunia zinapiga kelele za kuendelezwa usitishaji vita na kukomeshwa kikamilifu hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Palestina, lakini Wazayuni wahalifu na wanaoua watoto wanaota ndoto za alinacha za kufidia kushindwa kusikoweza kufidika kwa kuua raia, watoto na wanawake wasio na hatia.

Tags