Jan 16, 2024 07:05 UTC
  • Iran na India zatiliana saini makubaliano ya mwisho ya maendeleo ya bandari ya Chabahar

Waziri wa Barabara na Maendeleo ya Miji wa Iran na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India wamekubaliana kuendeleza Bandari ya Chabahar, iliyoko katika mkoa wa Sistan na Baluchistan, Kusini Mashariki mwa Iran.

Katika mkutano na mazungumzo ya Jumatatu, Mehrdad Bazrpash, Waziri wa Barabara na Maendeleo ya Miji wa Iran, na Subrahmanyam Jaishankar Waziri wa Mambo ya Nje wa India, pande hizo zilifikia makubaliano ya mwisho juu ya maendeleo ya bandari ya Chabahar.

Kwa mujibu wa Wizara ya Barabara na Maendeleo ya Miji, Mehrdad Bazrpash" alipendekeza kuundwa kwa kamati ya pamoja ya usafirishaji kati ya Iran na India ili kupanua ushirikiano kati ya pande hizo mbili na kusema: "Kuundwa kwa kamati hii ya kazi kutaamsha uwezo wa usafiri na kutumia ukanda wa kaskazini-kusini."

Kwa upande wake, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa India pia amesisitiza utayarifu wa nchi hiyo kwa ajili ya uwekezaji mpya katika nyuga za usafiri na uchukuzi nchini Iran.

Bandari ya Chabahar

 

Moja ya mipango ya maendeleo ya serikali ya Iran katika bandari ya Chabahar ni kuendeleza awamu ya pili ya bandari ya Shahid Beheshti na utoaji wa vifaa vya kimkakati vya kuboresha uwezo wa upakuaji na upakiaji.

Bandari ya Chabahar daima imekuwa na umuhimu mkubwa katika ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa wa eneo. Kwa upande wa jiopolitiki, Chabahar inahesabiwa kuwa bandari pekee ya bahari nchini Iran ambayo ni nukta muhimu katika Ukanda wa Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman ambayo kimsingi ina nafasi muhimu na ya kistratejia katika korido ya Kaskazini-Kusini.

Tags