Nasser Kan'ani: Jeshi la SEPAH ni mbeba bendera ya kupambana na ugaidi
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, mpango wa Bunge la Kanada wa kuwatangaza Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni magaidi ni hatua isiyo ya busara, ya kiuadui na kinyume na viwango na kanuni zinazokubalika za sheria za kimataifa.
Nasser Kan'ani Chafi amelaani hatua hiyo ya Wabunge wa Canada na kusema kuwa, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ni mshika bendera ya mapambano dhidi ya ugaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, mpango wa Bunge la Canada wa kulitangaza Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni la kigaidi ni hatua ya uadui na ni uingiliaji wa masuala ya ndani na ni mfano wa kuhujumu mamlaka na usalama wa taifa wa Iran.
سثحشا
Kanani ameongeza kuwa: Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na vikosi vingine vya jeshi la Iran lina jukumu la kulinda usalama wa taifa na mipaka ya nchi na vilevile kuchangia katika kuleta usalama na uthabiti wa eneo kwa kukabiliana na matukio ya ugaidi.
Kan'ani amewashauri wabunge wa Canada kuchunguza nafasi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ili kufahamu ukweli halisi wa mambo.