Sep 10, 2024 07:06 UTC
  • Shahram Irani: Iran haiogopi kukabiliana na dola lolote

Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa nchi hii imefikia kiwango cha nguvu za aina yake ambazo zinaifanya iweze kuchukua hatua mkabala wa hujuma na makabiliano mbalimbali dhidi yake.

Admeri Shahram Irani amesema nguvu na heshima iliyonayo hii leo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiwezi kulinganishwa na kipindi kingine chochote. Kamanda Shahram alibainisha haya  jana alipotembelea kituo cha mafunzo cha kikosi cha nchi kavu katika mkoa wa Tehran. 

Amesema, jeshi tukufu la Jamhuri ya Kiislamu haliogopi kukabiliana na jeshi au mamlaka yoyote ya kikanda na nje ya eneo katika Ghuba ya Uajemi. 

Kamanda wa jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiii vimekuwa vikijitokeza vyema na kwa wakati muafaka katika kila hatua zinazohitajika.

Jeshi la wanamaji ambalo lilikuwa likiishia tu katika Ghuba ya Uajemi katika miaka ya mwanzo baada ushindi wa Mapinduzi sasa limepata mafanikio ya kustaajabisha kiasi kwamba jeshi hilo sasa lipo katika maji ya kimataifa.

Jeshi la majini la Iran 

Kamanda huyo wa Iran ameashiria pia namna kikosi cha kivita cha wanamaji wa Iran kilichotumwa katika Ghuba ya Aden kilivyofanikiwa kukamilisha oparesheni zake salama salimini bila ya kupata ajali yoyote. "Ndio maana nchi kama Marekani zimeshindwa kukwepa mashambulizi yanayotekelezwa na makundi ya muqawama katika eneo dhidi ya meli zao ili kudhamini usalama wa meli hizo licha ya kuwa na meli nyingi za kisasa katika eneo", amesema Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Tags