Iran yaitaka EU iachane na sera zake chovu za vitisho, mashinikizo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya, na hasa Troika ya Ulaya E3 (Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza) kuachana na "sera zao zilizochoka" za vitisho na mashinikizo.
Katika ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X leo Ijumaa, Araghchi amegusia matamshi yaliyotolewa katika mazungumzo ya pamoja ya simu na mawaziri wa mambo ya nje wa E3 na Mwakilishi Mkuu wa EU katika Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama, Kaja Kallas.
Sayyid Araghchi ameashiria namna Washington ilivyojiondoam kwenye makubaliano ya nyuklia yaJCPOA na kueleza bayana kuwa, "Ilikuwa ni Marekani iliyojiondoa kwenye mkataba uliojadiliwa kwa miaka miwili, ulioratibiwa na EU mwaka 2015- na wala sio Iran."
Mwandiplomasia huyo mkuu wa Iran amesema katika mazungumzo hayo ya simu kwamba, ni Marekani vile vile iliyojiondoa kwenye meza ya mazungumzo mwezi Juni mwaka huu na kukhitari chaguo la kijeshi badala yake, na wala si Iran.
"Mazungumzo yoyote mapya yanawezekana tu wakati upande mwingine uko tayari kwa makubaliano ya nyuklia ya haki, yenye uwiano na yenye manufaa kwa pande zote," ameongeza Araghchi.
"Ikiwa EU au E3 wanataka kuwa na jukumu, wanapaswa kutenda kwa uwajibikaji," mwanadiplomasia mkuu amesisitiza, akiwataka wakuu hao wa Ulaya kuweka kando sera zao chovu za vitisho na mashinikizo, ikiwa ni pamoja na vitisho vya kuhuisha mchakato wa kuirejeshea Iran vikwazo vya Umoja wa Mataifa, mchakato ambao hawana kabisa msingi wa kimaadili na kisheria kuufufua.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa vikali misimamo isiyofaa inayochukuliwa na baadhi ya nchi za Ulaya ya kuunga mkono jinai za utawala ghasibu wa Israel katika eneo. Araghchi ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji na Waziri wa Mambo ya Nje Maxime Prévot leo Ijumaa.