Imam wa Swala ya Ijumaa Tehran: Maadui watakabiliana na makombora mapya ikiwa watafanya makosa
-
Haj Ali Akbari
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: "Iwapo maadui watafanya kosa jingine, watakabiliana na vita vipana zaidi badala ya vita vya kikanda, na badala ya kuzuiliwa Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati huo Mlango Bahari wa Bab al-Mandeb pia atafungwa.
Akihutubia katika Swala ya Ijumaa iliyohuidhuriwa na maelfu ya watu mjini Tehran, Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari amesema: Ikiwa watashambulia miundombinu yetu, tutashambulia miundombinu yote ya washirika wao katika eneo la Magharibi mwa Asia."
Imam wa muda wa Ijumaa wa Tehran, ameashiria vikwazo, mzingiro wa kiuchumi na vita vya utambuzi vya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu na kusema: Leo, badala ya kutumia risasi, maadui zetu wamezuia vyanzo vya mapato vya nchi kupitia vikwazo dhidi ya mafuta, benki na biashara.
Amesema kwamba tafiti zote za kisayansi, mafundisho imara ya kidini, na uzoefu wa kimataifa unaonyesha kwamba njia bora na isiyo na gharama kubwa ya kukabiliana na vita hivi vya kihistoria ni "usimamizi mzuri wa matumizi na kuongeza tija," akifafanua kwamba: "Kujiepusha na israfu si tena pendekezo la kimaadili au sifa ya kibinafsi, bali ni wajibu wa kidini na haja ya kimkakati ya kuilinda Iran, kumkasirisha adui na kushinda changamoto zilizopo."
Akizungumzia "Jihadi ya kujiepusha na israfu," Imam wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: "Kuwepo katika Jihadi hii ni kushiriki katika uwanja muhimu sana wa mapambano, na adui anadhani anaweza kutudhuru katika eneo hili."
Katika sehemu nyingine ya hotuba zake za Swala ya Ijumaa, Hujjatul Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari amezungumzia maendeleo ya kihistoria na hali ya sasa ya taifa la Iran na kusema, fikra ya "Umagharibi" na "Kuathiriwa na Umagharibi" imefeli katika taifa la Iran, akisisitiza kwamba: "Wairani wameelewa vyema kwamba mtindo wa maisha wa Magharibi si kigezo bora cha maendeleo, bali ni njia ya kudhalilisha mataifa. Uchumi wa kukopa na usalama wa kuazima wa Magharibi umetoweka kama sarabi."
Akizungumzia vitisho vya maadui, Hujjatul Islam Haj Ali Akbari amesema: "Vikosi vyetu vya jeshi viko tayari zaidi kuliko hapo awali, na mikono iko kwenye kitufe cha kufyatulia risasi. Maadui wajinga wana ndoto za uongo vichwani mwao. Ikiwa ndivyo ilivyo, basi mpira uko uwanja mwao."
Akiashiria vitisho vya Marekani kwamba machaguo yote yako mezani, Imam wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema: "Kwa sasa meza yanu imevunjika, mikono yenu inatetemeka na hamna tena machaguo. Sasa, taifa kubwa la Iran ndilo lenye machaguo. Mara hii mkifanya jambo la kijinga, mtaona Iran tofauti."
Akinukuu kaulu ya mmoja wa waliohudhuria ibada hiyo ya Swala ya Ijumaa, Haj Ali Akbari amewaambia maadui wa Iran kwamba: "Huu si wakati wenu. Mtu huyu muovu na mchafu yaani (Donald Trump) atauawa na kupelekwa Jahannamu na mmoja wa waathiriwa wa kambi ya Jeffrey Epstein."