Uchaguzi wa Iran una taathira kubwa zaidi kieneo
(last modified Wed, 24 Feb 2016 07:31:43 GMT )
Feb 24, 2016 07:31 UTC
  • Uchaguzi wa Iran una taathira kubwa zaidi kieneo

Mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kisiasa amesema uchaguzi wa Iran ni muhimu katika eneo

Sa'dullah Zarei mchambuzi wa masuala ya kisiasa Iran katika makala aliyoandika kwenye gazeti la Kayhan chapa ya Tehran amesema, moja ya sababu za kuwa na taathira uchaguzi huu ni matukio ya eneo.

Dkt. Zarei amesema Iran ambayo ina msimamo wa kimapinduzi kwa kutegemea uwezo wake wa ndani inajitahidi kukabiliana na madola ya kibeberu na makundi yanayofungamana na mabeberu.

Mchambuzi huyo wa mambo amesema maadui wa Iran kimataifa na kieneo wanaoutazama uchaguzi kama alama ya adhama na kuendelea mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Wairani milioni 54, wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa Ijumaa wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran na Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Masanduku 129,000 ya kupigia kura yamewekwa katika vituo 53,000 vya kupigia kura kote Iran. Aidha zaidi ya maafisa nusu milioni watasimamia zoezi la uchaguzi mwaka huu. Kampeni za uchaguzi zitamalizika Alhamisi hii, siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi.

Tags