Shamkhani: Baadhi ya nchi zinapanga kumimina magaidi Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i28146-shamkhani_baadhi_ya_nchi_zinapanga_kumimina_magaidi_afghanistan
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, kuna baadhi ya nchi za eneo hili zinafanya njama za kuharibu hali ya amani na kudhoofisha muundo wa kiusalama wa Aghanistan kama njia ya kuandaa mazingira ya kuwahamishia nchini humo magaidi walioshindwa katika nchi za Iraq na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 23, 2017 03:26 UTC
  • Shamkhani: Baadhi ya nchi zinapanga kumimina magaidi Afghanistan

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, kuna baadhi ya nchi za eneo hili zinafanya njama za kuharibu hali ya amani na kudhoofisha muundo wa kiusalama wa Aghanistan kama njia ya kuandaa mazingira ya kuwahamishia nchini humo magaidi walioshindwa katika nchi za Iraq na Syria.

Ali Shamkhani alisema hayo jana usiku wakati alipozungumza kwa simu na Mohammad Hanif Atmar, mshauri wa usalama wa taifa wa Rais wa Afghanistan na sambamba na kulaani shambulio la kundi la Taleban katika kambi ya kijeshi ya Afghanistan huko Balkh amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari ktoa msaada wowote unaotakiwa kwa waathiriwa wa shambulio hilo.

Vile vile amesisitizia udharura wa kuwa kitu kumoja serikali na makundi ya kisiasa pamoja na wananchi wa Aghanistan katika vita dhidi ya magaidi na kuongeza kwamba, kuna haja ya kuharakishwa ushirikiano wa kiusalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Afghanistan kwani hiyo ni ngao ya usalama na utulivu wa nchi hizi mbili ndugu na jirani.

Mohammad Hanif Atmar, mshauri wa usalama wa taifa wa Rais wa Afghanistan

 

Kwa upande wake, Mohammad Hanif Atmar, mshauri wa usalama wa taifa wa Rais wa Afghanistan ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misaada yake kwa Afghanistan na kuhimiza kuendelea mashauriano baina ya nchi hizi mbili hususan katika vita vya kutokomeza vitendo vya kigaidi.

Ikumbukwe kuwa wanajeshi 150 wa Afghanistan waliuawa siku ya Ijumaa baada ya kundi la Taleban kushambulizi kambi ya jeshi ya nchi hiyo karibu na Mazar Sharif, makao makuu ya mkoa wa Balkh wa kaskazini mwa Afghanistan.