Rouhani asisitizia udharura wa kufuatwa njia na malengo ya Imam Khomeini
(last modified Sun, 04 Jun 2017 08:02:41 GMT )
Jun 04, 2017 08:02 UTC
  • Rouhani asisitizia udharura wa kufuatwa njia na malengo ya Imam Khomeini

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito kwa watu wa matabaka yote kujifunza kuhusu malengo, azma na maono ya Imam Ruhullah Khomeini MA, muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Rais Rouhani aliyasema hayo jana jioni katika dhifa ya futari hapa jijini Tehran na kuongeza kuwa, kuna udharura wa kufuatwa njia ya Imam Khomeini MA, Baba wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Dakta Rouhani aliyasema hayo kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 28 tangu alipoaga dunia kiongozi huyo mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Waombelezaji pembeni mwa Haram ya Imam KHomeini MA mjini Tehran

Kumbukumbu hiyo inafanyika leo kwenye Haram ya Kiongozi huyo kusini mwa Tehran, ambapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anatazamiwa kuhutubia umma wa wananchi watakaohudhuria. 

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi mwaka  1979 Milaadia kwa uongozi shupavu wa Imam Khomeini MA. Aidha Imam alibobea katika elimu ya dini na mbali na kuwasomesha wanafunzi wengi na kutoa hotuba nyingi za kihistoria, aliandika pia vitabu vingi.