Kiongozi Muadhamu: Ni wajibu kwa Umma wa Kiislamu kupambana na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i30998-kiongozi_muadhamu_ni_wajibu_kwa_umma_wa_kiislamu_kupambana_na_israel
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, kwa mujibu wa fiqhi ya Kiislamu, Waislamu wote wanawajibika kupambana na kupigana jihadi kwa kutumia njia zote zinazowezekana dhidi ya adui anayevamia na kukalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu; kwa msingi huo hii leo ni wajibu kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu kupambana na utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 26, 2017 16:29 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Ni wajibu kwa Umma wa Kiislamu kupambana na Israel

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, kwa mujibu wa fiqhi ya Kiislamu, Waislamu wote wanawajibika kupambana na kupigana jihadi kwa kutumia njia zote zinazowezekana dhidi ya adui anayevamia na kukalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu; kwa msingi huo hii leo ni wajibu kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu kupambana na utawala ghasibu wa Israel.

Ayatullah Khamenei ameyasema hayo leo alipohutubia Baraza la Idil Fitri lililowakutanisha pamoja viongozi, matabaka mbalimbali ya wananchi na mabalozi wa nchi za Kiislamu mjini Tehran na kutoa mkono wa Idi kwa Waislamu wote. Amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Waislamu ya kukataa kushiriki katika mapambano hayo ya jihadi na kusema kuwa, taifa la Iran liko makini na pevu katika kutekeleza wajibu na majukumu yake. Ameongeza kuwa: Ulimwengu wa Kiislamu unahitajia kuwa na umoja na mshikamano na kwamba aghlabu ya mataifa ya Waislamu yako pamoja na yanashikamana na kuwa, ni wajibu wa serikali za nchi za Waislamu pia kutekeleza majumu yao. 

Ayatullah Ali Khamenei 

Ayatullah Khamenei amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds na mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika medani za kulitetea taifa la Palestina ni mfano wa kujifaharisha wa umoja na mshikamano wa Kiislamu. Ameongeza kuwa: Hii ndiyo maana ya umoja na mshikamano wa Kiislamu, kuona Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Iran wakijitokeza kwa wingi mitaani wakiwa katika funga na saumu ya mwezi wa Ramadhani na kuonesha mshikamano wao na wenzao wa Palestina wa madhehebu ya Suni.

Baadhi ya wawakilishi wa nchi za Waislamu katika Baraza la Idi, Tehran

Amesisitiza kuwa, kupuuza na kulisahaulisha suala la Palestina ni hatari kubwa na kuongeza kuwa: Umoja na kujiepusha na mifarakano vina maslahi kwa nchi za Kiislamu na kwamba, kuna udharura wa kuzuia mipango ya kuufanya Umma upuuze na kusahau kadhia ya Palestina ambayo ni kadhia nambari moja ya Umma wa Kiislamu, kwa kushirikiana zaidi katika suala hilo.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, Tehran

Ayatullah Ali Khamenei amesema, migawanyiko na hitilafu ndiyo tatizo na jeraha kubwa linalousumbua ulimwengu wa Kiislamu. Ameashiria mapigano ya umwagaji damu yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu kama Yemen, Syria, Iran na kaskazini mwa Afrika na kusema: Kukaribiana kwa nchi za Waislamu na kujiepusha kutumia nguvu za jeshi dhidi ya kila mmoja wao  kunaoana na hekima ya Mwenyezi Mungu na kuna maslahi kwa nchi zote za Waislamu.

Rais Hassan Rouhani

Kabla ya hotuba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Baraza la Idil Fitri, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu alitoa hotuba fupi akilishukuru taifa na jeshi la Iran kwa kuendelea kusimama kidete mbele ya magaidi na kusema kuwa, jibu lililotolewa dhidi ya magaidi hao limedhihirisha sehemu ndogo tu ya nguvu na uwezo wa kujihami wa Jamhuri ya Kiislamu.