Mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi waanza Tehran
Mkutano wa 13 Kimataifa wa Kupambana na ugaidi maarufu kwa kifupi kwa jina la Kalkan umenza leo mjini Tehran ukijadili njia ya kukabiliana na janga hilo.
Mkutano huo unahudhuriwa na shakhsia mbalimbali wa kitaifa na kimataifa akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Abdul Ridha Rahmad Fadhly, kKmanda wa Jeshi la Polisi la Iran, Meja Jenerali Hussein Ashtari na Katibu Mkuu wa Polisi ya Kimataifa (Interpol) Jürgen Stock.
Mkuu wa Polisi ya Kimataifa nchini Iran Mas'ud Ridhwani amesema katika ufunguzi wa mkutano huo kwamba, unajadili jinsi ya kuunganisha pamoja juhudi na uwezo wa Polisi ya Kimataifa (Interpol), jinsi ya kugundua na kuangamiza magenge ya kigaidi na kukabiliana na vyanzo vya fedha vya ugaidi.
Ridhwani amezungumzia hatua zilizochukuliwa na Polisi ya Kimataifa tawi la Iran katika uwanja huo na kuongeza kuwa: Interpol tawi la Iran imechukua hatua muhimu sana kwa ajili ya kutimiza malengo ya taasisi hiyo.
Mkutano wa sasa wa kimataifa wa kupambana na ugaidi unahudhuriwa na wawakilishi wa zaidi ya nchi 30 duniani.