Jul 19, 2017 14:30 UTC
  • Rouhani: Marekani haiwezi kusimamia haki za binadamu na uthabiti duniani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Marekani kwa kupuuza na kukanyaga makubaliano ya kimataifa iliyoyatia saini yakiwemo makubaliano kati yake na Paris, Cuba, Amerika ya kaskazini na Asia ya Mashariki haiwezi kusimamia haki za binadamu, sheria,amani na usalama duniani.

Akizungumza leo katika kikao cha baraza la mawaziri, Rais Hassan Rouhani  ameashiria hatua isiyo sahihi ya Marekani mkabala na makubaliano ya kimataifa na kuongeza kuwa, Marekani imepuuza makubaliano yake mengi hivi karibuni na kwamba nchi ambayo yenyewe haina uthabiti haiwezi kuheshimu sheria au makubaliano yoyote; na kwa msingi huo haistahiki kutoa mwito wa amani, uthabiti na utulivu kwa nchi nyingine.  

Rais Rouhani katika kikao na baraza la mawaziri mjini Tehran

Rais Rouhani amekutaja kuwepo Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati kuwa kumeshadidisha hitilafu na mapigano na kuongeza kuwa kujitolea  wananchi wa Iraq, Syria na nchi jirani pamoja na wanamuqawama kumelinusuru eneo hili na ugaidi na kwamba katika siku zijazo pia  eneo la Mashariki ya Kati litanusurika kutokana na uovu wa ugaidi. 

Rais wa Iran ameashiria pia kushindwa njama za Marekani za kuituhumu Iran kuwa imekiuka makubaliano ya JCPOA na kueleza kuwa Iran itaendelea kuheshimu makubaliano yake ya kimataifa, hata hivyo amesema viongozi wa Marekani wanataka kuiwekea Iran vikwazo vipya kwa visingizio mbalimbali katika hali ambayo Iran haijakiuka kivyovyote makubaliano ya JCPOA. Amesema Iran itatoa jibu linalofaa kwa Marekani iwapo nchi hiyo inataka kuiwekea Iran vikwazo kwa  anwani na kisingizio chochote.  Mkuu wa Mhimili wa Utendaji wa Iran amesema kuwa taifa la Iran limepata mafanikio makubwa na ya aina yake katika historia ya kisiasa ya Iran na kutetea haki zake mbele ya madola makuu ulimwenguni baada ya kufikia makubaliano ya pande kadhaa na ya kimataifa.

Tags