Brigedia Jenerali Hajizadeh: Iran ina "baba wa mabomu yote"
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i34427-brigedia_jenerali_hajizadeh_iran_ina_baba_wa_mabomu_yote
Kamanda ngazi za juu wa jeshi la Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina "baba wa mabomu yote" na lenye nguvu kubwa zaidi kuliko yote yasiyo ya nyuklia duniani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 16, 2017 03:47 UTC
  • Brigedia Jenerali Hajizadeh: Iran ina

Kamanda ngazi za juu wa jeshi la Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina "baba wa mabomu yote" na lenye nguvu kubwa zaidi kuliko yote yasiyo ya nyuklia duniani.

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amesema mabomu hayo yanaweza kurushwa kutoka kwenye ndege aina ya Ilyushin na yana nguvu kubwa 

Hajizadeh ambaye ni Kamanda wa kikosi cha anga na anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameashiria pia madai ya Marekani kwamba ina bomu kubwa kabisa lijulikanalo kama "mama wa mabomu" (MOAB) na kueleza kuwa, Iran ina "baba wa mabomu yote" na kwamba kwa maagizo ya kikosi cha anga na anga za mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, sekta ya ulinzi nchini imetengeza mabomu kadhaa ya aina hiyo yenye uzito wa karibu tani 10.

Bomu la mama wa mabomu yote la Marekani MOAB lenye uzito wa kilo 9,800 ambalo Marekani ilidai kuwa ndilo lenye nguvu kubwa kuliko yote yasilo ya nyuklia duniani lilitumiwa na nchi hiyo kupiga mahandaki ya chini ya milima katika mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan.

Iran inasisitiza kuwa uwezo wake wa kijeshi ni kwa ajili ya kujihami na si tishio kwa nchi nyingine.

Kombora la masafa ya kati la Iran likitumwa kuelekeza Syria

Mwezi Juni mwaka huu Iran ilirusha makombora kadhaa ya balestiki ya masafa ya kati ya dhidi ya ngome za Daesh katika mkoa wa Dayr al-Zawr huko Syria na kuangamiza wapiganaji zaidi ya 170 wa kindi hilo la kiigaidi.

Shambulizi hilo lilifanyika baada ya wapiganaji wa Daesh kushambulia majengo ya Bunge mjini Tehran na kuuawa watu 18.