Zarif asisitiza kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Senegal
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i42850-zarif_asisitiza_kuimarishwa_ushirikiano_wa_kiuchumi_kati_ya_iran_na_senegal
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria nyanja za ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Senegal na kusisitizia kuimarishwa na kustawishwa uhusiano wa pande mbili hizo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Apr 09, 2018 02:41 UTC
  • Zarif asisitiza kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Senegal

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria nyanja za ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Senegal na kusisitizia kuimarishwa na kustawishwa uhusiano wa pande mbili hizo.

Muhammad Javad Zarif ambaye leo Jumatatu amewasili Dakar mji mkuu wa Senegal kikiwa ni kituo cha kwanza cha ziara yake ya kuzitembelea nchi kadhaa za Afrika na Amerika ya Latini  amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, Iran ina uhusiano mzuri na Senegal katika nyanja mbalimbali. Katika ziara yake hiyo nchini Senegal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mbali na kufanya mazungumzo ya kisiasa na kuhusu masuala ya kieneo na viongozi wa nchi hiyo, anatazamiwa kushauriana nao pia juu ya masuala ya kiuchumi na kuzidisha mashirikiano katika sekta ya uchumi. 

Akiwa mjini Dakar Senegal, Zarif atakutana na kufanya mazungumzo na Rais, Spika wa Bunge na Waziri wa Mambo ya Nje. Aidha atashiriki kwenye kikao cha kamati ya pamoja ya kiuchumi kati ya Iran na Senegal. Akitoka Senegal, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ataendelea na ziara yake huko Brazil, Uruguay na Namibia.