Jun 14, 2018 08:04 UTC
  • Meja Jenerali Baqeri: Natumai amani na utulivu utatawala katika ulimwengu wa Kiislamu

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ana wingi wa matumaini kwamba karibuni hivi amani na utulivu utashuhudiwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Meja Jenerali Muhammad Hossein Baqeri amayesema hayo katika ujumbe wa salamu za Iddul-Fitr, aliowatumia maafisa wa majeshi ya nchi za Kiislamu jana Jumatano.

Amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu kwa maslahi ya mataifa ya Kiislamu kote duniani.

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, kuimarishwa uhusiano wa kidugu miongoni mwa nchi za Kiislamu na majeshi ya nchi hizo kutatoa mchango mkubwa katika kuzima njama za maadui wa Uislamu na Waislamu.

Umoja wa Kiislamu

Meja Jenerali Muhammad Hossein Baqeri ameongeza kuwa, ni kutokana na ushirikiano huo tu wa kidugu, ndipo Waislamu kwa pamoja wataweza kuzima njama za maadui dhidi ya mji mutukufu wa Baitul Muqaddas (Jerusalem), huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Waislamu kote duniani wanatazamiwa kusherehekea sikukuu ya Iddul-Fitr kesho Ijumaa, iwapo mwezi utaandama hii leo.

Tags