Apr 09, 2016 16:07 UTC
  • Brigedia Jenerali Hussein Dehqan, Waziri wa Ulinzi wa Iran
    Brigedia Jenerali Hussein Dehqan, Waziri wa Ulinzi wa Iran

Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein Dehqan amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje ya wa Marekani John Kerry kutafakari kabla ya kutamka maneneo ya “kipuuzi” kuhusu masuala ya kijeshi na kiulinzi ya Iran.

Akizungumza leo Jumamosi, Dehqan amekosoa vikali matamshi ya hivi karibuni ya Kerry kuhusu mpango wa makombora ya kujihami ya Iran. Amesema mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani anapaswa kutafakari kwa muda wa angalau dakika chache kabla ya kutoa matamshi ya kipuuzi yaliyojaa uchambuzi ghalati.

Siku ya Alkhamisi Kerry alisema, Marekani itafungua “mpango mpya” na Iran kwa lengo la kufanya mazungumzo kuhusu majaribio ya makombora ya balistiki ya Iran.

Dehqan aidha amelaani hatua ya Marekani ya kuendelea kuingilia mambo ya ndani ya nchi zingine duniani. Waziri wa Ulinzi wa Iran aidha amesema iwapo Marekani kweli inataka utulivu duniani basi inapaswa kuondoa vikosi vyake katika maeneo mbali mbali ya dunia na pia ikomeshe uungaji mkono wake kwa makundi ya kigaidi.

Tags