IMO yaipongeza Iran kwa kulinda usalama baharini na kukabiliana na maharamia
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Masuala ya Bahari, IMO, Kitack Lim, amepongeza nafasi ya Iran katika kukabiliana na maharamia na kulinda usalama wa maji ya Bahari ya Hindi na Ghuba ya Aden.
Lim ameyasema hayo leo Jumamosi mjini Tehran katika sherehe za Siku ya Usafiri wa Baharini Duniani na kwa mnasaba wa mwaka wa sabini tokea kuanzishwe Shirika la Kimataifa la Masuala ya Bahari, IMO. Ameongeza kuwa, Iran imeweza kupata mafanikio mazuri katika ustawi wa sekta ya meli na usafiri baharini na pia imeweza kuwa athirifiu katika kupunguza matukio ya maharamia ya kuhujumu meli za biashara.
Lim ameongeza kuwa, mwaka 2021 Iran itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa IMO na kuongeza kuwa kikao hicho kitabainisha umuhimu wa Iran katika sekta ya usafiri wa baharini.
Hadi kufikia Septemba mwaka jana Meli za Kivita za Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilikuwa zimesindikiza zaidi ya meli 4,200 za kibiashara katika eneo linalosumbuliwa na maharamia la Ghuba ya Aden na Bahari Hindi tokea mwaka 2008. Aidha tokea mwaka huo hadi hivi sasa Iran imetuma misafara zaidi ya 55 ya meli zake za kivita kulinda doria katika maeneo mbalimbali duniani. Amesema hivi sasa manowari za Jeshi la Majini la Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi.
Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Masuala ya Bahari, IMO, amesema, pendekezo la baadhi ya nchi za kutaka kuakhirishwa mpango wa kuzishurutisha meli za kibiashara zitumie mafuta yasiyo na sulphur na kusema mpango huo utaanza kutekelezwa mwaka 2020.