Mkutano wa Shirika la UN la Utalii wafanyika Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49474-mkutano_wa_shirika_la_un_la_utalii_wafanyika_iran
Mkutano wa 40 Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii duniani (UNWTO) ulianza Jumapili katika mji wa Hamedan magharibi mwa Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 12, 2018 23:22 UTC
  • Mkutano wa Shirika la UN la Utalii wafanyika Iran

Mkutano wa 40 Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii duniani (UNWTO) ulianza Jumapili katika mji wa Hamedan magharibi mwa Iran.

Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvili, na  Makamu wa Rais wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Turathi za Utamaduni, Ali Asghar Mounesan.

Katibu Mkuu wa UNWTO amesema lengo la kufanyika mkutano huo ni kubadilishana mawazo baina ya wanachama ili kuimarisha utalii duniani.

 

Vilevile ameashiria vivitio vingi vya utalii nchini Iran na akatabiri kuwa sekta ya utalii nchini ina mustakabali mwema. Aidha ameashiria vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema vikwazo kama hivyo huzifanya nchi kuwa na uwezo mkubwa zaidi. Amesisitiza kuwa UNWTO itaarifisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama nchi salama ya kitalii.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Makamu wa Rais wa Iran ambaye pia ni Mkuu wa Shirika la Turathi za Utamaduni, Ali Asghar Mounesan amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina taathira. Vilevile amebaini kuwa idadi ya watalii imeongezieka nchini Iran licha ya kuwepo vikwazo hivyo.

 

Mkutano wa 40 wa Wanachama wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unafanyika nchini Iran katika mji wa Hemedan kuanzia Novemba 12-14 na unahudhuria na wanachama 80 kutoka nchi 30 duniani.