Rais Rouhani: Vikwazo havina athari yoyote kwa uuzaji mafuta ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49511-rais_rouhani_vikwazo_havina_athari_yoyote_kwa_uuzaji_mafuta_ya_iran
Rais Hassan Rouhani amesema: Vikwazo batili na vya kidhalimu vya Marekani havina athari yoyote kwa uuzaji mafuta ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2018 12:41 UTC
  • Rais Rouhani: Vikwazo havina athari yoyote kwa uuzaji mafuta ya Iran

Rais Hassan Rouhani amesema: Vikwazo batili na vya kidhalimu vya Marekani havina athari yoyote kwa uuzaji mafuta ya Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kuongeza kuwa: Marekani ilikuwa ikidhani itakata kikamilifu usafirishaji nje wa mafuta ya Iran, lakini mwishoni imefahamu kwamba jambo hilo halitekelezeki wala haliyumkiniki.

Rais Rouhani amesema, kutokana na masuala ya ndani ya Marekani na bei ya mafuta, haiwezekani kukata usafirishaji nje wa mafuta ya Iran  na akasisitiza kwamba: Serikali ya Iran ina njia nyingi za upitishaji kwa ajili ya kuuza mafuta, ambazo haziwezi kuathiriwa na vikwazo.

Ameongeza kuwa: Licha ya mashinikizo yote na vikwazo vyote vilivyopo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeendelea kuwa na mawasiliano ya kifedha kimataifa. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Wananchi wa Iran watasimama imara kukabiliana na njama za Marekani na watazishinda njama hizo; na walimwengu wote wamebaini kuwa Marekani imezusha madai potofu, imefanya propaganda potofu na imekuwa ikifuatilia malengo ambayo haitayafikia katu.

Rais Rouhani amekumbusha tena kwamba: Marekani haiheshimu sheria na kanuni za kimataifa na inazikiuka sheria hizo.../